Kilimo kwa njia ya Mungu



Kilimo kwa njia ya Mungu ni aina ya kilimo ambacho mtu hulima eneo dogo kwa kufunika ardhi na kupata mazao mengi. Kilimo hiki ni kizuri na hasa kwa maeneo ambayo kuna mvua hafifu kwani matandazo yanayofunika ardhi ya Mungu huhifadhi unyevunyevu.

Faida za kilimo hiki
1. Kuhifadhi unyevunyevu katika udongo hasa kwa maeneo ambayo mvua ni chache
2. Matandazo yanapooza, hutengeneza mbolea (Compost) ambayo baadae hurutubisha ardhi
3. Hutumia eneo dogo kulima na kuvuna mavuno mengi
4. Ardhi haichoki maana ina chakula cha kutosha
5. Hufunika ardhi ya Mungu.
N.B kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu, tulime kwa maendeleo yetu.https://www.yumpu.com/en/document/read/26550765/farming-gods-way-facilitators-study-guide

0 Comments

Newest